Sababu za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.

1.Umri mdogo wa kikomo cha maisha (life expectancy)

Kama unafahamu hili jambo utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa Sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko wanaume zao.

2.Ugumu katika kufunguka

Wanaume wengi ni wagumu sana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu  kwenye ndoa mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.

3.Ugumu katika kusamehe

Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali kw afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingi tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona.

4.Tabia hatarishi

Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi,anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu Zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanonii mkoani.

5.Ugumu katika kujali afya

Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

6.Msongo wa mawazo

Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusiimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Kwanini ndoa Nyingi huvunjika mapema

Mpenzi msomaji wa makala zetu pendwa napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha tena katika safu hii ya Mapenzi na mahusiano. Kama ndio umepakua Application Hii leo hujachelewa, Bado mambo ya kujifunza ni mengi sana.

Tumekua tukiona ndoa nyingi sana duniani zikifungwa kwa mbwembwe kubwa mno kiasi kwamba wawili hao hawatakuja kuachana. La hasha! Sikweli. Leo nakuletea siri kubwa zinazopelekea ndoa hizo hizo unazoona hazitakufa kuvunjika kwa haraka.

Moja kwa moja sipendi kuwachosha sana Huwa nawaletea TIPS hizi zipo wazi kabisa naimani utagungua mapungufu na changamoto za ndoa zilivyo.

1.Kwa sasa hakuna Mapenzi bali kuna biashara ya mapenzi, Kwanini nasema biashara ya mapenzi sasaivi watu wanaangalia maslahi kwanza then mambo mengine baadae hivyo kama huna pesa gari na nyumba lazima uachwe tu.

2.Wanawake kujitambua. Sasa hivi sio kama enzi za nyuma, wanawake wengi wameelimika hivyo kuwa na ufahamu wa kujua haki zake kama mwanamke ila wanawake wa zamani wengi walikuwa hawapelekwi darasani hivyo haki nyingi za mwanamke zilikuwa zimejifunga hazijulikani. Mwanamke wa zamani alikuwa anajua kuwa ni haki yake kupigwa, kuonewa na mwanamme ila wa sasa hivi baada ya kuelimishwa na sheria kufuata mkondo wanawake wengi wameamka. Nafasi ile ya mwanamke kuvumilia kipigo imekuwa hakuna tena hivyo akikutana na mwanamme huyu mwenye tabia ambayo inavunja haki za mwanamke anajua jinsi ya kujitetea na hivi ndivyo wanaume weengi hawapendi na kupelekea ndoa kuvunjika.

3. Wanawake wa nyuma wengi walikuwa ni golikipa akae nyumbani asubiri mume ndio amuhudumie kifedha na matumizi ila wanawake wa sasa wengi ni watafutaji hivyo kupelekea yale manyanyaso ya wanaume waliyokuwa wakiwapa wanawake kisa ni kumhudumia sasa mwanamke hakubali. Mwanaume alikuwa anauwezo wa kufanya lolote kwa mkewe kwa gia ya kwamba atamnyima fedha za chakula n.k. hivyo mwanamke alikuwa hana budi awe mpole asikose anavyohitaji yeye na watoto.

4.Kutokana na Biashara za Kimataifa, Utandawazi wanawake na wanaume wamekuwa wakiiga tabia za Magharibi na za nchi nyingine sababu kwa sasa imekuwa ni rahisi sana kumuona Rihana msichana mrembo kavaa nini, je kapendeza kuliko enzi hizo ulikuwa huwezi ona picha wala video hizi kwani hata luninga ilikuwa unalipia sehemu kuangalia, Simu za mkononi zenye mtandao hakuna hivyo utakayemuona hapo karibu Role model wako anakuwa ni jirani yako au mtu katika Familia yako.

5.Sasa hivi wanawake na wanaume wamekuwa wakishiriki sana katika tendo la ndoa kabla ya kuoa na kuolewa. Hivyo pale anapoingia katika ndoa hakuna jipya analoenda kuliona. Ila enzi za nyuma ilikuwa mume na mke mnaowana bado hata tendo la ndoa hamjakutana. Mume ndio kwaanza anayemvunja bikira mkewe na kupelekea kuwa na mapenzi moto moto, kuona kitu kigeni ndani ya miili yenu.

USISAHAU: SHARE APP HII KATIKA MAGROUP YA WHATSAPP NA FACEBOOK ELIMU HII IWAFIKIE WOTE.