Mambo yakufanya mpenzi akichepuka.

Msomaji wangu, katika maisha ya kimapenzi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa kunakouma zaidi ni pale unapobaini mpenzi wako kampa penzi mtu unayemjua halafu ukijilinganisha wewe na huyo aliyepewa unashindwa kuelewa kilichomshawishi mpenzi wako.

Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake.

Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimedhibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako amechepuka na kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.

Mtaalam wa masuala ya mapenzi James Johnson kutoka Marekani amependekeza mambo 10 unayoweza kufanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.
Kubaliana na kilichotokea
Kama kashakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

Usijalaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema ‘najuta kumkubalia awe mpenzi wangu’. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempata basi uchukue kisha uufanyie kazi.

Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

Mpasulie ukweli
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni ‘msanii’ na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

Msamehe
Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.

Iwe fundisho kwako
Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

Kwa njia hizi lazima apagawe

Umekuwa na wakati mgumu hivi karibuni kufurahia ngoma kila siku? Mambo haya yatasaidia kuwasha tena moto wa mapenzi na kukuwezesha kufika kileleni mara kwa mara!

1: Usilenge kileleni, kuna mlima wa kukwea Bidii nyingi kitandani si kiungo pekee cha kumtosheleza mwanamke; kila unapotia bidii ndivyo matokeo yanadidimia. Badala yake, tumia ujuzi zaidi; zingatia shughuli si shabaha. Kushiriki mapenzi si mashindano; achana na hesabu na ujivinjari!
2: Mwili wako kipimo tosha Mwili wako ni kipimo tosha kukuambia iwapo mambo ni shwari au la – acha kufuata kile ambacho mawazo na moyo unakuambia. Weka kando wasiwasi na uzime mijadala akilini mwako. Jifunze kubaini hisia na ashiki za mwili wako, na uzipatie usukani kama inavyotakiwa. Ni baada tu ya kujua kinachozuzua mwili wako ndipo utamwelekeza mwenzio maeneo atakayobonyeza. Habari Nyingine: Maneno sita ya kumfurahisha mpenzi wako
3: Weka kila kitu wazi Baada ya kubaini kinachozuzua mwili wako, jadili na mpenzi wako. Mwanzoni, mjadala huu hautakuwa rahisi lakini ndiyo njia ya pekee kwa yeye kupata ramani ya mwili wako. Usihofu, muambie kila kiungo kinachokuzuzua na atakushuru sana.
4: Imarisha ngoma Mambo mapya huleta uchangamfu na msisimko wa kipekee chumbani. Tupa nje mitindo ya zamani kumbatia mapya! Soma majarida kisha ujadiliane na mpenzi wako mitindo mipya utakayodondoa hapo, asije akadhania umetumbukia katika ponografia ama kuna jamaa anamfunza moja kwa moja. Habari Nyingine: Sababu nne kuu za wanandoa kulala pamoja
5: Kuwa na imani Kila kitu hutendeka kwa imani, hata kushiriki mapenzi. Uko na haki zote za kujivinjari; Mungu mwenyewe aliumba ngono kwa sababu anataka ufurahie mahaba!

Ukiwa na sifa hizi kwenye ndoa utaishi miaka mingi

Mara nyingi tunapofikiria namna ya kumpata mwenza sahihi, huwa tunaangalia ishu ya kumpata yule mwenye mapenzi ya dhati lakini kumjua anayekupenda kwa dhati, anayeweza kukupatia kile ulichokitarajia ni vigumu sana.

Ndiyo maana hapa chini nimekupa vigezo saba vya mtu ambaye anakupenda kwa dhati na anafaa kuwa mwenza wako endapo mtakuwa tayari mmeshaanzisha uhusiano wa kawaida.
MGUSO WA HISIA
Hakika mapenzi ni mguso wa hisia, kwa maana hiyo kigezo kikuu cha kuzingatia kwa mtu anayestahili kuwa mwenzi wako wa ndoa ni vile ambavyo hisia zake umeziteka. Hali kadhalika na wewe mwenyewe ulivyotekwa naye.
Amani na furaha vikitawala kati yenu unajiona upo huru kwa kila kitu na mnapokuwa hamuelewani kila kitu kwenye akili yako unaona hakiendi. Vivyo hivyo na yeye kwamba amani ipo pale mnaelewana na inatoweka mnapokosana. Huyo ni wazi mnaendana.
KUTOSHEKA

Ukiwa naye unajisikiaje? Umetosheka eeh? Akiwa mbali inakuaje, unahisi kuna upungufu mkubwa? Vipi na yeye anajiona hivyohivyo? Kama jibu ni ndiyo maana yake mnaendana kwa sababu ukamili wako unamtegemea yeye, hali kadhalika na yeye.

Anakata kiu yako yote? Na upande wake inakuaje? Ikiwa ni hivyo, basi anatosha kuwa mwenzi wako wa maisha.
MALENGO

Kila mtu anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo lake huwa ni kudumu. Achana na hulka za viruka njia. Pointi hii inakujenga kujua matarajio ya mwenzako kuhusu wewe. Anakuhitaji kwa maisha yake yote au yupo na wewe kwa sababu hana pa kwenda?

Wengi wapo kwenye majuto kwa sababu waliingia kwenye ndoa na watu ambao hawakuwa na nia ya dhati nao, bali walijichanganya baada ya kukosa uelekeo.
ISHU YA MAWASILIANO

Anapenda kuwasiliana na wewe, ukimtumia SMS anaijibu ‘fasta’. Hatengenezi sababu ya kutowasiliana na wewe, daima anaona njia pekee ya kuwaweka karibu hata kama mpo mbali ni kuwasiliana. Nawe unampigia simu kwa wakati, unasikia raha kupokea ujumbe wake naye anaona fahari kupigiwa simu na wewe.

Kama hali hiyo ipo, basi upendo wa kweli upo na hiyo inatosha kuthibitisha kwamba mnaendana. Ukituma SMS naye akachelewa kujibu ni wazi haoni umuhimu wako.
NI WA SHIDA NA RAHA

Hapa ni hisia tu, ikiwa mnapendana kwa dhati basi akiumia nawe yatakuwa ni maumivu yako. Ikiwa hauna raha halafu yeye ni mwenye furaha basi huyo anakupenda kinafiki. Hatofautiani na yule anayebembeleza ndoa ili kuondoa mkosi. Kuwa makini, hakikisha unakuwa na mtu ambaye ni wa shida na raha.

ANAJUTA NA KUOMBA MSAMAHA

Mpenzi bora ni yule anayejutia kosa pale anapokukosea, pia anaomba msamaha. Hapa ieleweke kuwa kuomba msamaha peke yake haitoshi, isipokuwa anapaswa kuonesha wazi kwamba ametambua makosa yake na amejuta.

Kimsingi mtu mwenye sifa hiyo huwa hasumbui mnapokuwa ndani. Epuka mtu mbishi, anakosea na hatambui kosa lake na badala yake anajenga hoja.
HAYUKO TAYARI KUKUKOSA
Mnagombana anaumia lakini bado yupo na wewe. Anakuonesha waziwazi kuwa hayupo tayari kuachana nawe. Yupo radhi kutumia muda mwingi kutafuta suluhu ili muendelee kuwa pamoja. Hiyo inaonesha kuwa anakupenda kwa moyo mmoja.
Mtu mwenye moyo mgumu, mnagombana wala hashtuki na hatengenezi mazingira ya kurudiana, maana yake hana hisia za kweli, na anavyokuchukulia ni kwamba hata mkiachana yeye anaona sawa.
JIANGALIE NA WEWE!

Umeangalia yote hayo, sasa jiangalie na wewe mwenyewe. Moyo wako unakusukuma kuwa na yeye? Hilo ndilo swali la msingi kwa sababu mapenzi hayataki majaribio, ukiingia ndiyo imetoka. Yanini kujipa kumbukumbu mbaya baadaye?

Maisha bora au mabaya ya baadaye yanatokana na uamuzi wa leo, mwenzi sahihi wa maisha ni mbolea ya furaha ya kudumu baadaye. Kwa hiyo kabla hujaingia kwenye uhusiano wa ndoa ni vema kujiuliza mara mbilimbili.