Bibi ananishawishi nimuoe Huyu Mwanamke aliyenitafutia.

Robo ya Maisha yangu niliishi Moshi-Kibosho, kuanzia Std 1-form 1. Kwa muda wote nimekuwa nikiishi na bibi.

Sasa Tangu nije hapa kwake kuna binti huwa anakuja hapa nyumbani anasaidia saidia kwani kuna shughuli mbalimbali zinafanyika .

Mimi sikumtia maanani, na nilijua anaweza kuwa moja ya ndugu zangu kwani tuliokuja huku ni wengi . Ni binti mdogo kama miaka 20 hivi, mwembamba black beauty na karefu hivi.

Sasa jana nikiwa na jamaa zangu tuliokuwa tumeachana kitambo tukipiga stori mbilitatu na mbege taratibu, ndipo Akaja mdogo wangu kuniambia bibi anakuita.

Nilimkuta bibi kabeba Mundu (Panga flani limepindwa mbele) akaniambia nikamsaidie kubeba mkungu wa ndizi shambani.

Tukiwa tunatembea, akaanza kuniuliza maswali ninaoa lini? Au ninataka afe ndio nioe asimuone mjukuu wake na Moli wake (mke wangu)?

Nilimweleza kuwa bado naweka mambo sawa, na nina muhaidi hatakufa kabla ya kuona hivyoo vyotee.

Akaniuliza Mchumba umeshampata, nikamjibu bado huku najichekeshaa.

Bibi alikuwa mbele, ndipo akageuka nyumna na kunieleza, unamuona yule binti wa fulani?

Nikawa sijampata mana mabinti huku ni wengi. Akanieleza binti mwenyewe alivyo, na kuniambia, tayari ashamwambia Mama yake kuwa anataka Mjukuu wangu(mimi) amuoe binti yake….

Akasema ndio maana yupo hapa tangu umekuja. Akaniambia kamaliza form 4 hakufaulu lkn akiwa hapa kijijini, hakuwahi jihusisha na tabia mbaya, anajua kukata majani ya Ng’ombe, kufagia zizi la ng’ombe anajua kulima, kufanya usafi, kupika na anakwenda sana kanisani.

Akasema kazi zote za nyumbani hufanya yeye, na watu wa hapa kijijini wanampenda sana. Akasema niachane na vibinti vya mjini kwani ni vivivu na havijui kufanya kazi na haviogopi mungu.

Kiukweli aliongea mengi lkn kubwa ni msisitizo kuwa nimuoee. Nilimjibu tutaongea na nitafikiria kwa kuzingatia kuwa, haitakuwa busara kumkatalia au kuanza kubishana nae.

Ilinibidi nianze kufuatilia nyendo za huyu dogo na nikagundua kuwa, hata yeye alikuwa tayari alikwishwa elezwa mpango huu.

Anyway, mkasa ndio huo, kuhusu kuoa au kutomuoa hilo sintalizungumza hapa ila habari kubwa niliyokutana nayo Kibosho ndio hii.

One Reply to “Bibi ananishawishi nimuoe Huyu Mwanamke aliyenitafutia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *