Mambo yakufanya mpenzi akichepuka.

Msomaji wangu, katika maisha ya kimapenzi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa kunakouma zaidi ni pale unapobaini mpenzi wako kampa penzi mtu unayemjua halafu ukijilinganisha wewe na huyo aliyepewa unashindwa kuelewa kilichomshawishi mpenzi wako.

Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake.

Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimedhibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako amechepuka na kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.

Mtaalam wa masuala ya mapenzi James Johnson kutoka Marekani amependekeza mambo 10 unayoweza kufanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.
Kubaliana na kilichotokea
Kama kashakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

Usijalaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema ‘najuta kumkubalia awe mpenzi wangu’. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempata basi uchukue kisha uufanyie kazi.

Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

Mpasulie ukweli
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni ‘msanii’ na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

Msamehe
Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.

Iwe fundisho kwako
Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

MKASA: House girl utanimaliza

Nipo kwenye lindi la mawazo kuhusu housegirl wetu ambae nilimpa mimba kwa bahati mbaya. Mimi nina mke na familia yangu huyu binti sasa anataka nimfanyie kitu mbaya maana mimba hataki kuitoa na kuondoka kagoma na muda unazidi kwenda mwishowe itaanza kuonekana

Sasa hivi anashinda kwenye TV tu na remote kazi hataki kufanya yote tisa, kumi sasa juzi Jumamosi usiku katumwa kazi na wife unaambiwa kamfanyia wife kiburi kisichosemekana katumwa akalete kitu dukani akakataa live akaambiwa akapike akakataa, akaanza kuongea kwa mafumbo huku akienda chumbani mimi nilikua bar kwenye mambo yangu.

Mdogo wangu wa kike ndio akazifanya zile kazi nyumba imekua very tense bomu linaweza kulipuka any time wife anamwandalia pesa zake aweze kuondoka maana kwa mawazo ya wife anadhani kwa kuwa hatujamlipa mshahara miezi mitatu mfululizo ndio maana analeta kiburi kumbe ni mimba.
Sijui niongee na Chale akodi wavuta bangi! Wakuu kati yenu kuna mwenye jawabu ya hili tatizo? Hivi kwanini huyu binti ananifanyia hivi!? Kwanini asikubali kupokea hela akaondoka, kila nachomwambia hataki, anasema eti nitamwacha, sasa Mimi simtaki tena, kwa nn tunalazimishana?
Wanaume wapo kibao why me? Wangapi wametoa mimba hawajafa? Mke wangu mwenyewe alishika mimba huku tuna mtoto mchanga wa miezi sita mbona aliitoa na hakufa? Sasa yeye ni nani hasa asitoe, mi naona nikodi wahuni tufanye elimination method.
Wadau nyumba inaungua naomba kwa imani zenu wote mniombee naahidi sirudii tena nikipona na janga hili maana wife wangu hanaga mchezo kabisa na mambo ya uzinzi msg tu ya simu alitaka kuniacha huko nyuma.Kuna mganga anaeweza kubadilisha matokeo ya tatizo kama hili?

USHAURI: Boyfriend wangu anataka wakati mimi bikra.

Mambo! Mwalimu wa Mapenzi. Naimani kupitia Makala zako nitapata msaada wa mawazo tafadhali.

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23,naishi kigamboni,nimemaliza chuo mwaka jana.

Nina Tatizo linanisumbua,nashukuru Mungu nimeweza kuvumilia kwa muda mrefu bila kulala na Mwanaume.Nimeweza kuhifadhi zawadi nzuri yenye thamani kubwa ambayo kwa mwanamke mwenye Heshima zake anastahili awe nayo kwa ajili ya kumpa mume wake baada ya kufunga Ndoa(namaanisha kuwa mie bado bikra).

Tatizo Linalonisumbua ni kwamba kila muda Boyfriend wangu ananisumbua anataka nifanye nae mapenzi,nikimnyima anasema kuwa simpendi,na kiukweli mi nampenda tena sana,na ninajisikia vibaya ninapomuona mpenzi wangu amenuna amekosa furaha,

Kwani hakuna Njia nyingine ya kumfanya aniamini kuwa nampenda bila kufanya nae mapenzi?

Ninachotaka mimi Nimpe Penzi kwenye Usiku wa Fungate kama Zawadi Special kwa ajili yake lakini Naogopa nikiendelea kumnyima nahisi ataniacha au atanisaliti akapate ninachomnyima kwa wanawake wengine.

Naombeni Ushauri Nifanyeje?

MKASA; Nilimtega Mume wa dada na amezama katika mahusiano

Hi Mwalimu Wa Mapenzi.

Naitwa Tayana mbulula nipo Mbezi Dar es salaam, naombeni ushauri wenu wasomaji wa makala za Mwalimu wa Mapenzi.
kuna mume wa dadangu nampenda sana kwani ana sex body na ni handsome boy sana, yaani six packs zake nakufa kabisa.
Huyu shem wangu anaishi Lusaka na dadangu, mwezi mmoja uliopita nilienda kumtembelea dada na nikaanza kujitongozesha kwa shem na ilifikia hatua nadondosha taulo mbele yake ili kumtega,
Kuna kipindi dada alisafiri na nikautumia muda huo kumshawishi tufanye mapenzi akakubali na tukawa tunafanya mapenzi mpaka mara 4 kwa siku,
Sasa nimerudi home na siku zangu sizioni nimepima nina mimba ya shemej yangu, nimemwambia shem kakubali na kanisifia mi mtam kushinda dadangu,
Sasa anataka nimwachishe na dada anioe mimi, nami nampenda.

NISHAURINI NITUMIE NJIA GANI WAACHANE HARAKA NAMI NIWEZE KUOLEWA NA SHEMEJI.??

Dalili 5 Kuu za Mwanamke Anayetaka Kuachana na wewe.

Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo wa kuficha mawazo yake.

Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.

Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.

Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.

1. Hupenda kujitenga.
Mwanamke ambaye anapenda kujitenga na mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali za kuelekea kuachana naye. Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai penzi. Hoja inabaki pale niliposema yeye kushindwa kuamua haraka na hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.

2. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Mwanamke ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake yuko kwenye hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.

Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.

3. Hupenda kukosoa kila kitu.
Kama nilivyosema, kujua historia ya penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo muhimu kwa sababu husaidia kujua kama kuna mabadiliko hatari ya tabia za mwanamke.

Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.

4. Kutokukutegemea
Mwanamke ambaye ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa alikuwa anakuomba nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine atasitisha bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri uwezekano wa kukuacha wakati wowote.

5. Kupunguza mawasiliano.
Asikwambie mtu aiseeeh, mapenzi ni mawasiliano bora kati ya mume na mke. Endapo itatokea ya kwamba hakuna mawasiliano thabiti baina yako na mpenzi wako kama ambavyo ilikuwa mwanzo basi tambua fika penzi lenu limefika ukingoni.

Hizo dalili chache kati ya nyingi za mwanamke ambaye anataka kuachana nawe katika muhusiano ya kimapenzi.

Bikra ni lazima damu itoke? Majibu yote haya hapa.

KUTOKA KWA MDAU:

Habari Mwalimu wa Mapenzi, natumaini wewe ni mzima wa afya.
Nimekua nkifuatilia application yako kwa ukaribu sana umekua ukitufundisha mambo mengi sana ambayo hata mie sikua nikiyafahamu hapo kabla. Pole sana kwa majukumu.

Mimi ninatatizo na nimeona wewe ni wapekee ambae unaweza kunisaidia tatizo langu, siku za karbuni nilipata mpenzi ambae aliniambia kua yeye ni bikra nilikubali kwa hilo.

Lakini siku ya siku nilifanya nae mapenzi ikiwa ni siku ya kwanza alilalamika sana anaumia ikabidi tuache, siku ya pili tukafanya tena kwa bahati nzuri uume wangu ulifanikiwa kuingia ndani vizuri na tukamaliza tendo kwa amani.

Lakini wasiwasi wangu naona kama amenidanganya coz marafiki zangu waliniambia kuwa unapofanya mapenzi na bikra lazima atoke damu kuashiria bikra yake imetoka.

Mpenzi wangu hajawahi kutoka damu sasa sielewi naona kama ananicheat, naomba unisaidie dada yangu kwani nilazima mwanamke bikra atokwe na damu katka tendo la ndoa ikiwa ndo mara yake ya kwanza?

**********

MAJIBU YAKO MPENZI MSOMAJI WANGU WA MAKALA MBALIMBALI:

Namshukuru Mungu kwa uzima na afya njema. Ahsante kwa ushirikiano.
Umenikumbusha hadithi za magazetini enzi zile nipo shule….msimulizi anaandika “Nikamlaza, nikaanza mnyonya nini na nini kisha nikaingiza…Binti akalia sana kwa maumivu, nilipomaliza nikakuta shuka lote limelowa kwa damu”….

Hiyo ni fantancy, Bikira haloweshi shuka kwa damu unless katikati ya tendo Hedhi ikaanza, au wakati wa tendo Binti kuvunja ungo (inawatokea mabinti wadogo wanaolazimishwa kuolewa/bakwa) au umefanya kwa fujo sana mpaka ukamjeruhi mtoto wa watu au umembaka.

Enzi zile, Usiku wa Harusi/kutolewa Bikira Shangazi/Bibi/Kungwi anakuja na kijitambaa cheupe na kukipachika Ukeni ili kujua kama Bikira imetoka. Kwamba kukiwa na Damu shangwe, kikiwa kisafi Kilio.

Lakini kumbuka enzi zile Mabinti wengi waliolewa wakiwa wadogo na bila mapenzi so technically walikuwa wakibakwa na wengine kuvunjishwa Ungo kabla ya siku zao hivyo Damu ilikuwa ndio ushuhuda pekee!!

Pale ukeni (unapoingia uume/inapotoka damu ya Hedhi) huwa na kijiutandu ambacho kinaweza kutoka kutokana na shughuli za kimaisha au mtindo wa maisha.

Mf: Binti kufanya shughuli ngumu/za kutumia nguvu katika umri mdogo (kulima, kubeba maji, kupanda ngazi (watoto wa maghorofani mpo hehehehe).

Pia michezo, mfano Mpira, kuruka kamba, kuendesha Baiskeli n.k kunaondoa kile kijiutandu ambacho wengi ndio huesabu kuwa ni Bikira.

Ukweli ni kuwa, Bikira ni kutokufanya tendo la ngono (kutoingiliwa na mwanaume).

Nikijibu swali lako…. Hapana! Sio lazima damu imtoke mwanamke mara yake ya kwanza kufanya mapenzi.

Siku inayofuata baada ya tendo anaweza kuona uchafu uliochanganyikana na damu kwenye chupi ikiwa aliumia….inategemea ulimuingilia kwa nguvu kiasi gani.

Hali hiyo inaweza kuendela kwa siku mbili-tatu kisha akawa poa, again sio lazima kuwe na damu.
Mapendo tele kwako.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

MKASA: Mke wangu anataka tufanye mara tatu.

Wakati watu wanalalamika wanakosa haki yao ya ndoa lakini kuna wengine wanakinai kabisa. Loh! Mapenzi yanaendesha dunia jomoni.

Kutoka kwa Msomaji wa Makala zetu:

Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama 3 zilizopita amekuwa akinilazimisha nile mzigo kila siku hapa nilipo kichwa kinaniuma kutokana na kazi ya kila siku ya kuhakikisha anafurahi na jana nimeona nivunje ukimya baada ya kuniamsha usiku wa manane nile mzigo, nikamueleza mke wangu utaniua naomba tupumzike hata siku tano mbele target yangu ni kuwa baada ya siku tano anatarajia kuingia kwenye siku zake hivyo nitapata mapumziko ya kutosha.

Cha ajabu mke wangu kaanza kulia na kulalamika kuwa haamini kauli yangu ya kukataa kula mzigo, ilinibidi nimbeleze kisha nikampoza na kamoja hapa nilipo nipo njiani natoka job ameshanitumia sms ananiambia eti niwahi Anahamu ya dushe langu nimekaa kimya sikumjibu kanipigia simu anasisitiza alichokiandika kwenye sms yake tena kwa sauti ya majonzi.

Nampenda mke wangu ila ananichanganya kwa vile tabia hii hakuwa nayo mi ndio nilikuwa initiator wa mchezo wetu.

Hebu wadau wa App ya Mwalimu wa Mapenzi naombeni mnisaidie itakuwa kapatwa na nini hadi amekuwa hivi? Tabia hii kaanza tangu niliporudi kutoka safarini ambapo nilikaa kule kwa miezi 3 bila kushiriki nae.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Jinsi ya kumjibu mpenzi anapouliza ‘Unanipenda Kiasi Gani?’

Uh its another day. Mambow wapenzi wasomaji wa makala zetu, karibuni kwenye jamvi letu tena lililotandikwa kwenye kona maridhawa ya mapenzi.

Hii ni kona iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kujuzana mambo mawili matatu kuhusu masuala ya mahusiano ya mapenzi ambayo ‘yanafanya dunia izunguke’ bila sisi kujua tunazunguka nayo.

Wapo waliowahi kusema mapenzi ni ‘ukichaa’ kwa sababu kila wakitafakari baadhi ya matukio waliyoyafanya kutokana tu na kupenda wanaamini hawakuwa katika hali ya kawaida kiakili! Lakini wapo wanaoamini hakuna hisia nzuri na zenye busara iliyopitiliza kama hisia za mapenzi ambazo hazifichiki hata akipewa ‘bingwa wa kuficha siri za dunia’.

Anyways, tuweke kando hizo blabla leo tuangazie swali ambalo karibu kila mmoja aliwahi kuuliza ama kuulizwa na mpenzi wake au hata mtu anayemshawishi kuwa mchumba. “Baby, unanipenda kiasi gani?” ni swali la mtihani ambao ulishavuja karibu kwa kila mtu, lakini hata anayeliuliza huwa hajui majibu.
Hivyo, wa kuliwekea alama hutegemea tu kile anachosikia, hata kama sio sahihi anaweza kuweka alama kubwa ya ‘vema’.

Wakati unajibu swali hili, nakushauri usihangaike hata kidogo kutafuta vipimo unavyovijua wewe hata kama ni kipimo cha ukubwa wa dunia na bahari zote. Picha itakayojengeka kichwani kwa unayemwambia itakuwa ya ‘kusadikika tu’.

Usilijibu swali hili kama unavyojibu maswali mengine ya kawaida anayokuuliza, jaribu kutengeneza kwanza mazingira mazuri ya haraka ya kuishika akili yake. Mvute zaidi umakini uwe kwako. Macho yako na muonekano wako uonekane kweli unataka kujibu swali muhimu la mapenzi sio mtihani wa mwalimu ‘Kabuche’. Lol. Hapo utakuwa umetengeneza mazingira ya ushindi.

Mwite jina zuri mwanzo, mfanye ajisikie anaongea na mpenzi, kama mko wawili mshike mkono taratibu, nyuso zitazamane… macho yako yatakusaidia kuzungumza zaidi kinachoelezwa na mdomo.
Kama wewe ni muongeaji sana, sauti yako ishuke kidogo iwe ‘romantic’. Hii ni kwa sababu moyo wa muuliza swali hupanuka na akili yake hutamani kusikia neno zuri sana kutoka kwako ambalo hata yeye halijui… hivyo inategemea utamwambia nini.

Angalia baadhi ya majibu yanayoweza kufaa, sio lazima uyakopi haya yangu… chukua kama mfano.

Tafadhali sana narudia, usitafute kufananisha nyota, bahari, mchanga na vingine, hii ni dunia ya dijitali na hiyo ilikuwa mifano ya zamani, huenda isimsisimue sana. Ni kama stori ya kunywa maji na kukuona kwenye bilauli!

1. “Baby, ingawa hakuna kifaa cha kupimia kiasi cha mapenzi, naamini mapenzi hayapimwi kwa maneno bali vitendo. Na hakuna ajuae kipimo cha tendo zaidi ya mtendewa. Kipimo cha mapenzi yangu kwako ni wewe… matendo yangu yanaongea, naomba unipe alama nazostahili. Lakini naamini nakupenda kiasi kisichoelezeka lakini kile kinachougusa moyo wako ni sehemu tu.”

2.“Baby, nakupenda kiasi kwamba kwamba naamini siwezi kupenda zaidi ya hapa.” Hapa ni kama unasema kuna kipimo na ushafika mwisho wa alama husika.

3.“Naamini ni neno ‘upendo’ pekee linaloweza kuupima upendo wangu juu yako. Siwezi kusema ni kiasi gani kwa sababu ni vigumu kusimulia kwa uhalisia maumivu ya kidonda, lakini ninaamini hiki ninachokisikia juu yako ndio maana halisi na sahihi kabisa ya neno upendo uliokomaa.”

Hata hivyo, majibu kutoka kwa mtu asiyependa kweli yanaweza kumuumbua tu hata akiyasema vyema kwa sababu macho yanayongea zaidi ya mdomo kwenye mapenzi. Chukua hii.

Maneno matamu yaendane na matendo matamu, hapo ndio utaona kweli mapenzi hayana kiwango cha elimu.

Kumbuka kuchagua maneno kutakusaidia kudumisha penzi lako, usiropoke tu majibu kisa umemzoea mwenzio ama unataka kuonekana mjuaji sana, itakugharimu. Katika mapenzi kila alama ni muhimu kuliko hata umuhimu unaoujua, hata kicheko chako tu kinaweza kushusha alama. Beba mapenzi kwa umakini wa hali ya juu zaidi ya kutembea juu ya trey la mayai.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Jinsi ya kumwacha Mpenzi wako kwa amani.

Ziko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika.

Ama kwa amani ama kwa ugomvi.
Kumaliza mahusiano sikitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba.

Kumbuka “The Golden Rule”: Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:

1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya:

Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka “Maamuzi magumu”. Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto, maana utakuwa unachezea hisia zako.

2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano:

Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

3. Maliza Mahusiano Wewe Binafsi:

Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kipindi chochote ambacho uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo yakamalizwa na mwenyewe binafsi. Usitumie njia yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe, usitumie SMS, usitumie IM “Chat”, usitumie simu au email au barua au mtu yeyote kufikisha ujumbe. Ukitaka kumaliza mahusiano kwa amani, tafuta muda wa kukaa na mwenzi wako in person au face to face ili kuumaliza uhusiano huo katika hali njema.

4. Chagua Mahali Panapofaa.

Mahali pazuri panapofaa ni pale ambapo wewe unayetaka kumwacha mwenzako ungekuwa wewe unaachwa ungependa iwe mahali gani ili uelezwe? Be on his/her shoes. Public Places si mahali pazuri sana kwani mwenzi wako anaweza kujisikia kadhalilishwa. Kama ukiweza chagua mahali patakapomfanya mwenzi wako awe confortable na kurelax kama yuko nyumbani kwake.

Angalizo: Kama una uhakika kuwa mwenzi wako anaweza kuleta ukorofi, basi chagua Public Place kama kwenye restaurant ambapo wapo watu wengine. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kuleta vurugu. Public Place patakufanya ujiamini. Pale mambo yatakapochachamaa unaweza kuondoka tu bila tishio la ugomvi kwa kuwa kuna watu. Ukiona hali si shwari ni vema uanze kuondoka wewe kuliko yeye kuondoka kwanza.

5. Msikilize Mwenzi Wako:

Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako. Kumsikiliza mwenzi wako kutamfanya mwenzi wako atoe yote aliyokuwa nayo moyoni kitu ambacho kwa uhakika kitasaidia kumaliza mahusiano kwa amani. Pia unaweza kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika mahusiano yako yanayofuata.

6. Kuwa Mpole Na Dhibiti Hisia Zako:

Moja ya sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika ni pamoja na wahusika wote kutokuwa na furaha na amani na mwenzi wako. Wakati wa kuvunja mahusiano hayo pia yanaweza kujitokeza hasa pale mtakapoanza kulaumiana na kuonyeshana vidole ni nani mwenye makosa. Hakikikisha unadhibiti hasira hisia zako na hasira hata kama anachoongelea mwenzio kitakutia hasira. Ukifanya hivyo utafanikisha kuwa na mazungumzo ya amani.

7. Kuwa Mtulivu na Makini:

Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole. Kama kuvunjika kwa uhusiano wenu kutakuja kama Suprize kwa mwenzio, basi bila ya shaka atahitaji muda wa kuyameza unayomwambia, kuyatafakari ili aende sambamba na wewe katika mazungumzo yenu. Inaweza ikawa si habari njema kwa mwenzi wako kwa hiyo utulivu wako na upole katika maongezi yenu kutamfanya apunguze maumivu.

8. Mkimaliza Maongezi Ondoka Haraka:

Iko hivi: Kwa kiasi kikubwa anayeachwa anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa ataachwa kwa hiyo hatakuwa na furaha kwa yeye kuachwa. Anaweza akakulaani sana na kukuita majina yote mabaya anayoyajua na hivyo kukufanya na wewe uwe na hasira. Tulia. Jizuie. Kwa kuwa umeshaongea na pia umemsikiliza kistaarabu, huna haja ya kuendekeza ugomvi au malumbano. Ondoka. Hakuna faida utakayoipata kwa kuendelea kutoa maelezo yoyote ya ziada. Kama ni mwelewa na mmemaliza maongezi kwa amani basi mwage na nenda zako.

Je, ni nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano mbalimbali uliyopitia? Na je, kuna lolote la kujifunza ?

Jinsi gani Mwanamke anaweza kumfanya Mume wake akachepuka na shosti zake.

Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Lakini naomba leo niseme kwamba, wapo watu wanajitakia kusalitiwa na hapa nawazungumzia wanawake.
Kuna wanawake ambao wana wapenzi au wako kwenye ndoa lakini wanafanya mambo ambayo yanawafanya wasalitiwe kirahisi.

Unamkuta mke anachekelea mumewe kuwa na ukaribu na shosti wake, anajipenda kweli huyu? Hili ni tatizo na ndiyo maana leo nimeona nizungumzie mambo manne ambayo ukiyafanya lazima mumeo ‘atoke’ na marafiki zako.

1.Ukaribu wa mume na marafiki wa mke. Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao. Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?
Sisemi uanze kumfikiria tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo wamemchukua. Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia.

2. Mawasiliano ya mume na marafiki wa mke. Sisemi marafiki zako wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana kwa mambo gani?
Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea, walahi utaula wa chuya!

3. Mke kuanika siri za mumewe. Kuna hii tabia ya baadhi ya wanawake kuwasimulia mashosti zao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba! Eti unamkuta mke anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa faragha.
Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo. Kimsingi hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.Nne; mwanamke kutochukua nafasi yake. Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.
Hili liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza kumfanya akusaliti.
Hata kama wapo wanaopatiwa kila kitu lakini wanachepuka, hao ni wale wasioridhika na ni wachache. Wewe chukua nafasi yako kama mwanamke halafu hakikisha unaziba mianya ya mumeo kushawishika kwa wengine.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome