FUNZO; Maongezi ya Mke na Mume nani yupo sahihi hapa?

Mpenzi msomaji wa makala zetu najua utajiuliza sana kwa nini leo nimekuletea haya mazungumzo ya Mke na Mume ilihali ni mambo ya ndani sana. La Hasha! Najua wengi wenu mtapenda kujifunza kitu kutokana na Mazungumzo haya. Mazungumzo yenyewe ni kama ifuatavyo:

MKE: Naomba nilipe hela ninayokudai

MUME: Hela ipi mke wangu unayonidai?

MKE: Wiki iliyopita nilitumia hela yangu kumnunulia Sara madaftari, halafu juzi Rama alikuwa anaumwa nikamnunulia dawa kwa hela yangu, halafu wiki nzima mboga nimenunua kwa hela yangu. Hukuniachia hela yoyote uliposafiri kwenda kazini. Jumla nakudai 22,500. (Elfu 22 na 500)

MUME: OK, kwani Rama na Sara ni watoto wa nani?

MKE: Ni wangu mimi na wewe.

MUME: Kwahiyo, uliwauzia huduma ulizowapa mpaka nikulipe?

MKE: Hapana, lakini nilitumia hela yangu binafsi, nilipe mimi bwana

MUME: Nitakulipa, ila nikifa naacha wosia watoto wakalelewe kwa mama yangu mzazi.

MKE: Kwanini wakati nipo?.

MUME: Kwa kuwa utatumia hela yako kuwahudumia halafu utaanza kuwadai kwa vile huwa hudumii bure bali ni biashara. Halafu mke wangu hivi mimi hela nazotafuta ni za kwangu au ni za mimi na wewe na watoto? Hizo zawadi nilizowaletea wewe na watoto utanilipa kwa kuwa nimetumia hela yangu?

MKE: Lakini hela hiyo nili….

MUME: Wewe ni msaidizi wangu, ubavu wangu. Chako ni chetu, changu ni chetu. Nikikulipa tafsiri yake wewe ni mfanyakazi au hawara na si mke. Au una mume wa kumsaidia kutunza familia zaidi yangu?

MKE: Nipe hela yangu Baba Sara, la sivyo utajuta.

MUME: Na wewe lipa kodi ya nyumba yangu, la sivyo ondoka.

MKASA WA KWELI: Nilitaka kumuoa Lakini alinifanya Danga.

Napenda kuchukua nafasi hii kama msomaji wa makala za Mwalimu wa Mapenzi kwa kuweza ku-share mkasa wangu ambao nimeona utakua fundisho kwa vijana wa kiume kama mimi.
Niende moja kwa moja kwenye mkasa.
Date ya kwanza tulipata chakula cha jioni halafu tukawa tunatembea huku tunapiga stori. Tukapita karibu na supermarket akaomba kuna kitu nimnunulie, nikamwambia chukua chochote ntakununulia (hili jibu lilikua kosa kubwa)

Baada ya kuchukua cha kwanza, cha pili, akaona mikono haitoshi akaenda kuchukua basket kabisa. Nikawaza leo nimeumia lakini acha nimuangalie. Baada ya kumaliza tukaenda counter, bili ikasoma almost laki, nikamwona kashtuka kidogo. Labda alifikiri sikua na hiyo hela. Nikaingia mfukoni nkatoa noti za kutosha.

Wakati nahesabu akagundua pesa zipo, akaenda kuongeza kitu kingine. Tulipotoka nje akawa anawaza halafu akanambia kuna kitu amesahau anaomba akaongeze. Nikampa hela akaenda kuongeza. Alivyorudi tukachukua bajaji mpka kwao nami nikaondoka.

Kwa kuwa anakaa na dada yake ambae ameolewa nikafikiri atamuelekeza mdogo wake kuwa kitu alichofanya sio kizuri, tena siku ya kwanza. Matokeo yake ikawa kinyume kabisa, yani kila nikitoka na huyu mwanamke, dada yake anapiga simu anataka apelekewe chakula, tena vya bei mbaya. Wiki ikakatika nikawa nimetumia pesa nyingi zaidi ya ambayo natumia kwa mwezi. Mara kusuka na kuosha nywele, mara kuna kitu anataka anunue.

Kuna siku alinambia anataka nimnunulie smartphone, nikamkubalia na nilidhamiria kumnunulia. Lakini akaongezea kutaja kabisa simu anayotaka. Nikamwambia kama ni hiyo itabidi isubiri kwa kuwa ya gharama zaidi, akasema sawa.

Wikiendi akaja gheto, baada ya stori kidogo nikaanza kumuandaa. Akanizuia na kuniambia “mbona una haraka sana mimi”. Akanishangaa utafikiri nimefanya kitu cha ajabu, nami nikapotezea. Baadae akanambia nimuahidi kuwa sitamuacha. Nikamuuliza kwani umefanya nini mpka nikuache, akakosa jibu.

Kesho yake tukaonana tena, nikamwuliza kwa nini ananifanyia vitu kama vile hatuna future. Nikamwambia tubane matumizi, halaf sio lazima kila tukitoka achukue take away ampelekee dada yake. Akaja juu kuwa kama pesa watanirudishia. Nikamjibu sijawahi kuwa na mapenzi ya hivyo, mambo ya kudaiana vitu siwezi.

Kufupisha stori tumeshaachana. Pamoja na madhaifu yake ni mwanamke aliyeugusa moyo wangu. Amenipa furaha na huzuni ndani ya muda mfupi. Kama mtu angebahatika kutuona katika outings zetu asingeamini kama uhusiano wetu umedumu ndani ya wiki tatu tu.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp Groups. Share kote wenzio nao wasome

Madhara ya Punyeto kwa Wanaume

Madhara ya kupiga punyeto kwa wanaume

1. Punyeto hukufanya uwe dhaifu, inapoteza protini na kalsiamu ndani ya mwili wako.
2. Huleta matatizo kwenye neva nyurolojia ndani ya mwili
3. Ni moja ya kisababishi kikuu cha uhanithi (uume kushindwa kusimama)
4. Ni rahisi kuwa mtumwa wa kujichua (teja) unaweza kujaribu mara 1 tu na tayari ukawa teja wa jambo hilo kila mara
5. Huleta uchomvu sugu na kwa haraka zaidi, mara nyingi utahitaji kulala usingizi hata nyakati za mchana
6. Husababisha mfadhaiko (stress) kwenye akili na kwenye roho yako pia
7. Huleta matatizo ya kisaikolojia, hukusababishia majonzi na huzuni na kukufanya kujilaumu nafsi mara baada ya kumaliza kujichua
8. Punyeto haifanyiki kirahisi, unahitaji akili yako iwaze au itazame picha mbaya au chafu au kumfikiria kimapenzi mtu asiyekuwepo hapo ulipo. Hili ni jambo baya zaidi kwa afya kwani picha hizo hazikuondoki haraka kichwani mwako tofauti na ukishiriki tendo la ndoa na binadamu mwenzio moja kwa moja.
9. Punyeto inakupelekea kufanya makutano haramu kwakuwa hiyo hamu yako ya kutaka kujichua kila mara itakupelekea kuanza kutafuta vijarida au picha za ngono jambo ambalo ni baya zaidi kwa afya yako ya mwili na roho
10. Punyeto inapelekea tatizo lingine kubwa zaidi nalo ni kuwahi kufika kileleni utakaposhiriki tendo la ndoa na mwenza wako, hii itakuletea shida kwenye mahusiano yako wewe mwenyewe na hata kwa mwenza wako.
11. Punyeto inapunguza uwingi wa mbegu (reduces your sperm count) kama matokeo yake mwanaume hataweza kumpa mwanamke ujauzito. Hili la kuwa na mbegu chache ndilo chanzo kikuu cha ugumba kwa wanaume na ni matokeo ya kupiga punyeto mara kwa mara.
12. Kimaadili kabisa punyeto au kujichua ni jambo baya, unamuwaza fulani na kujikuta ukishiriki tendo la ndoa peke yako. Hii inapunguza thamani yako na nidhamu kwa wengine. Unaweza kuwa mzuri kwenye maeneo mengine mengi lakini utaishia kuwa na matatizo kama hutaiacha tabia hii haraka.
13. Punyeto inapoteza muda wako na kukufanya mtu usiye na faida
14. Raha ya kujichua haibaki akilini kwa kipindi kirefu kama vile ukishiriki tendo la ndoa kwa na mtu halisi
15. Punyeto husababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ni vigumu kuwa na akili ya utulivu na kukumbuka vitu kama tayari umeshakuwa teja wa punyeto.
16. Kujichua siyo soluhisho la mwisho la hitaji lako, yaani hutaona kuridhika katika kitendo hicho, kadri unavyofanya ndivyo unavyoendelea kuhitaji zaidi na zaidi mpaka mwisho unakuwa hanithi kabisa bila kujitambua
17. Punyeto haina faida yoyote kwenye maisha yako ya kimapenzi, huhitaji kwa ajili ya chochote
18. Punyeto inaongeza aibu, inapunguza uwezo wa kujiamini. Wengi waliozoea kujichua hata kutongoza kwao huwa ni kazi kubwa mno kiasi wengine huona bora kuendelea kujichua kuliko kutongoza mwanamke.
19. Utapoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa kirahisi zaidi kama utaendelea kujichua
20. Punyeto huchochea mapenzi ya jinsia moja hasa mashuleni, vyuoni na kwenye mahoteli na mwishowe hupelekea kusambaa kwa magonjwa mengi ya zinaa.
21. Punyeto inamaliza nguvu za kiume, kama unapenda kujichua basi sahau kuwa na nguvu za kiume. Upungufu wa nguvu za kiume ni janga la kitaifa miaka ya sasa lakini chanzo kikuu ni vijana wengi wa kiume kuanza kujichua tangu wakiwa mashuleni.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp Groups. Share kote wenzio nao wasome

Hiki ndio chanzo cha Mkeo Kutembea na Rafiki yako

Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.

Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilikuwa na kazi kubwa ya kumshauri rafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na rafiki yake.

Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambia wazi kwamba, amekuwa hapati penzi alilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.

Msichana huyo akaenda mbali zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia ngumu kukataa.
Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mpenzi wako bila kumdhihirishia kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.

Unapokuwa umeanzisha uhusiano na mtu, utambue ana watu wengi wanaomtaka lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali, hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako. Atachepuka na hata kama ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha.

Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mpenzi wako akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua.

Wewe mwenyewe
Endapo utakuwa umeanzisha uhusiano na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku.
Kwa mfano, endapo umekuwa na mpenzi wako lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mpenzi wako atahisi yeye ni mtu sahihi kwake.
Kujirahisi kwake
Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahisisha kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?
Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.
Kumuamini sana
Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.
Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mpenzi wako baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo.
Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa katika mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.
Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mpenzi wako aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukuwa mpenzi wako kwenye gari kumrudisha nyumbani.
Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mpenzi wako kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.
Rafiki mnafiki
Unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakuchukulia mpenzi wako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.
Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wapenzi wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa wapenzi wao au wapenzi wa mashoga zao.
Penzi la kweli
Mfano Juma ana mpenzi wake aitwaye Asha na Juma ana rafiki yake aitwaye Jamali. Juma na Asha ni wapenzi lakini hawapendani kivile ila Jamali anaonekana kuwa na penzi la kweli na Asha na wakati huohuo Asha naye anahisi kuwa na penzi la kweli na Jamali.
Katika mazingira hayo usije ukashangaa siku moja kusikia Asha katembea na Jamali. Siyo kutokana na tamaa au ushawishi bali ni kutokana na uwepo wa penzi la dhati kati yao.
Katika mazingira haya ndipo ambapo tumekuwa tukisikia fulani kamuacha mkewe kisha yule mke kaolewa na mwanaume ambaye alikuwa rafiki wa wanandoa hao.
Tamaa tu
Endapo utagundua mpenzi wako katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.
Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliyenaye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonyeshe mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia ukiwa na ujauzito

Ujauzito ni safari ndefu inayomchukua mwanamke miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua.

Ni safari yenye mikikimikiki na hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito kama jambo la kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke.

Ujauzito siyo hali ya hatari au kutisha endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi cha ujauzito hadi baada kujifungua. Katika kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.

Katika makala haya Mwalimu wa Mapenzi App tutazungumzia mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kubeba mimba, siyo kila mwanamke anaweza kubeba mimba kwa sababu wengine huwa na matatizo katika mfumo wao wa uzazi, aidha homoni zao hazifanyi kazi vizuri na mayai hayazalishwi au hayapevuki.

Huenda pia mirija ya uzazi imeziba au ana matatizo ndani ya kizazi.

NINI CHA KUFANYA?

Ni vyema upange sasa unataka kuwa mjamzito au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo, hakikisha umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako.

Mshirikishe mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri kushtukiza kwani inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja wenu hajajiandaa kisaikolojia.

CHEKI AFYA YAKO

Hakikisha una afya njema, huna magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo, kansa, HIV, kifafa, pumu, siko seli au group lako la damu ni RH negative.Endapo una matatizo haya hapo juu, basi haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe yatamwathiri mtoto.

Hakikisha huna magonjwa au matatizo katika viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu mbaya, vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri, matatizo katika mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la ndoa.

ACHA VILEVI

Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto.

Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya Folic Acid, ni vema ule sana mboga za majani au upate virutubisho vya Folic Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic Acid, kuna hatari ya kuzaa watoto wenye matatizo.

MAZOEZI

Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.

YANAYOKWAMISHA UJAUZITO

Matatizo yanayoweza kukusababishia usipate mimba ni kutofahamu siku za kupata mimba, kuziba mirija ya uzazi.Pia uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi na kwenye vifuko vya mayai. Uvimbe wa aina hii unaweza kutibika kwa dawa na ukaisha au kwa njia ya upasuaji, inategemea na daktari wako atakavyoona na kuamua.

Kwa upande wa wanaume wanaojiandaa kuwa wazazi, ni vema umjulishe mpenzi wako sasa unataka mtoto au lini unataka mtoto. Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa uzazi, mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa manii zote zinatoka ukeni.

Ni vema ukapime mbegu zako za kiume kuona kama zina ubora wa kutosha, usiwe na maumivu yoyote ya mwili kwani yataweza kukusababishia kupunguza nguvu za kiume na kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Zijue sifa kumi za mke mwema.

MKE MWEMA HUJAWA NA HEKIMA.

Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mwanaume anaempenda anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata mpaka marafiki wanatambua kuwa hali ni mbaya.
Ni vizuri kutofanya jambo kwa hasira na kuiruhusu hekima kukutawala.

UVIVU SIO SEHEMU YA MAISHA YAKE.

Kuna wanawake ambao ni wavivu kupita kiasi hawawezi fanya jambo lolote wenyewe lazima kumtegemea dada wa kazi. Kila kitu huwa wanakua na sababu utasikia sipigi deki sababu kiuno kina mshituko, sifui nguo kucha zangu ni laini zinakatika, hawakosi sababu kwa kile wanachotakiwa kufanya,ili uwe mwanamke/mke mwema jifunze kujibiidisha na uache uvivu.

NI MSAFI, ANAYEJUA KUPANGILIA MAVAZI YAKE

Kuna wanawake ambao wanaamini wanaume wanaangalia tabia tuu. Sio kweli. Lazima avutiwe na wewe kwanza maana tabia haionekani kwa nje ni kitu cha ndani,so mwonekano wako ndio unaoweza kumfanya kutaka kujua tabia yako. Mwanamke/mke mwema anajua avae nini kwa wakati gani na anajua namna yakupangilia rangi za mavazi yake ili kuonekana akiwa na mvuto, Mwanaume anapomwangalia mwanamke anapata picha hata ya watoto wake watakavokua wanavalishwa. Sio tu mavazi hata mwili- ni vizuri kuwa msafi wa mwili sio kijasho cha hatari au harufu isiyo kuwa ya kawaida, kumbuka Mungu ndo anaangalia moyo ila mwanadamu anaangalia nje kwanza moyo badae kwa hiyo usafi wa mazingira na mwili ni jambo muhimu.

ANATIMIZA MAHITAJI YA NDOA KWA MUME WAKE

Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku.” Kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipiza visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama anapanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

ANAJUA KUPIKA CHAKULA KITAMU CHENYE KUFURAHIWA NA FAMILIA.

Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani. Ni hatari mwanamke kuwaza ndoa wakati hata chai ukipika unaunguza

ANATAMBUA KUWA WIVU NA HISIA MBAYA NI ADUI WA NDOA YAKE.

Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo, sio unaita watu nakuanza kusimulia madhaifu ya mumemo.

ANA HOFU YA MUNGU SIYO YA MUME

Ni hatari sana kuwa na mwanamke mwenye hofu ya mwanaume na siyo ya Mungu. Hofu ya Mungu itamfanya asifanye vitu kwa kificho maana anauhakika Mungu anaona kila sehemu, Mwanamke mwenye hofu ya Mwanaume ni janga maana machoni kwa mwanaume ni mwema kama kondoo akitoka hapo ni mbuzi mwenye pembe kali. Wakati mwingine wanaume wamekua wakijitia moyo watawabadilisha hao wanawake. Kama hakubadilika mkiwa rafiki usitegemee atabadilika ndoani. Mke akiwa mcharuko uwezekano mkubwa wa watoto kuwa kama mama ni mkubwa maana ndo anakuwa nao muda mrefu

MWENYE MATUMIZI MAZURI YA PESA

Hili ni jambo la msingi sana na wanawake wengi huwa hawajui wanaume wengi huwatega katika huu mtego na kuwapima. Siku zote usitake kukomoa kwasababu anaekununulia ni mwingine na sio wewe, mtu katolewa labda chakula cha jioni ataanza kuagiza vitu alivyokua anaviona kwa tv bila hata kujua bei yake mradi halipi yeye, au kama ni shoping atahakikisha kanunua kila kitu alichokuwaga anawaza maishani bila kujali gharama kwa alie mtoa. Lakini pia hata kama ni kwa hela yako mwenyewe jifunze kuwa na akiba. Ni aibu sana mwanamke/msichana mwenye zaidi ya miaka 20 kutokua na akaunti/fedha ya akiba.

HUJISHUSHA NA KUOMBA MSAMAHA

Ugomvi mwingi kati ya mwanaume na mwanamke au mume na mke mara nyingi hutokana na wote kutaka kua juu hakuna aliyetayari kushuka. Kumbuka mwanamke ndio mlinzi wa ndoa. Wakati mwingine kushuka kwako ndio kunaweza pelekea mume/mwanaume naye kuona makosa yake lakini kutojishusha mara nyingi huleta magomvi ambayo mwishowe huleta aibu.

MWENYE MAWAZO YA KUENDELEZA FAMILIA.

Mwanamke mwenye upeo mpana wa kufikiri sio yule anaewaza namna ya kubadilisha ma dera, mwanamke mwema ni yule mwenye kukaa na kushauriana na mumewe juu ya mipango ya maendeleo na kumtia moyo mumewe juu ya mipango aliyonayo na sio kuwa kikwazo kwake na kumuonyesha kuwa hawezi kufikia malengo yake.

Zifahamu aina 10 za ndoa.

1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua
hawakuwa wakipendana!

2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume 18 mke 16. Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.

4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha
barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni
mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati.
Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.

9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu
ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza.
Kuwa mwangalifu!