Mwanaume mwenye malengo na wewe utamtambua kwa haya

Nipe nikupe imekuletea hapa Tabia za mwanaume mwenye malengo na wewe zisome…

1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.

2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.

3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!

4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!

5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.

6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!

7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.

Hizi ni baadhi ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii.

Hao wenye six pack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa milegezo, wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, waume za watu, masupa staa, watoto wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.

Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hizo pesa zake, hivyo na wewe unajiongeza kwenye foleni!

Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto njema, mapenzi ya kweli ni vigumu sana kuyapata. Ila pesa na mali ni rahisi sana kuzipata kama utajibidiisha.

Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! – Ukishikwa shikamana, ukipendwa, pendeka!