Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa


1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.

Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku atachoka, maana hana moyo wa jiwe bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na kupendwa katika maisha yao

SMS 9 zitakazokuletea furaha na faraja katika Mahusiano yako.

  1. Wangu kipenzi ninayekuenzi, jua wanitia uchizi na kuninyima usingizi, sijui kama una kizizi au ni mapenzi ndiyo yaninyima huo usingizi, la azizi nimekumiss kichizi, u hali gani mpenzi?
  2. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!
  3. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.
  4. Mpenzi najua u-mbali nami, majaribu ni mengi wapaswa kujihami, nituniye zangu zabibu wangu tabibu, jitahidi kuwa mvumilivu nitakuja kukutibu, miss u ma luv.
  5. Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kujyatibu, napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu, mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda.
  6. Nimeamini wewew ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunikamua, luv u.
  7. Kuwa nawe najivunia, mtoto mapenzi wayajua, kiuno, sauti yako tamu mithili ya chiriki wajua hasa kuitumia, mua wangu wajua kuukamua, ukiniacha jua nitaumia, nakupenda usije niacha nitajiua!
  8. Mambo yako adimu ndiyo yanayonipa wazimu, nikuonapo hupatwa hamu, hutamani unipatiye wako utamu, la azizini lini utakuja kunitoa hamu, hakika nimemiss wako utamu na kwa kuupata sifahamu, maana ni wewe tu ndiyo mtaalamu. Miss u

Bibi ananishawishi nimuoe Huyu Mwanamke aliyenitafutia.

Robo ya Maisha yangu niliishi Moshi-Kibosho, kuanzia Std 1-form 1. Kwa muda wote nimekuwa nikiishi na bibi.

Sasa Tangu nije hapa kwake kuna binti huwa anakuja hapa nyumbani anasaidia saidia kwani kuna shughuli mbalimbali zinafanyika .

Mimi sikumtia maanani, na nilijua anaweza kuwa moja ya ndugu zangu kwani tuliokuja huku ni wengi . Ni binti mdogo kama miaka 20 hivi, mwembamba black beauty na karefu hivi.

Sasa jana nikiwa na jamaa zangu tuliokuwa tumeachana kitambo tukipiga stori mbilitatu na mbege taratibu, ndipo Akaja mdogo wangu kuniambia bibi anakuita.

Nilimkuta bibi kabeba Mundu (Panga flani limepindwa mbele) akaniambia nikamsaidie kubeba mkungu wa ndizi shambani.

Tukiwa tunatembea, akaanza kuniuliza maswali ninaoa lini? Au ninataka afe ndio nioe asimuone mjukuu wake na Moli wake (mke wangu)?

Nilimweleza kuwa bado naweka mambo sawa, na nina muhaidi hatakufa kabla ya kuona hivyoo vyotee.

Akaniuliza Mchumba umeshampata, nikamjibu bado huku najichekeshaa.

Bibi alikuwa mbele, ndipo akageuka nyumna na kunieleza, unamuona yule binti wa fulani?

Nikawa sijampata mana mabinti huku ni wengi. Akanieleza binti mwenyewe alivyo, na kuniambia, tayari ashamwambia Mama yake kuwa anataka Mjukuu wangu(mimi) amuoe binti yake….

Akasema ndio maana yupo hapa tangu umekuja. Akaniambia kamaliza form 4 hakufaulu lkn akiwa hapa kijijini, hakuwahi jihusisha na tabia mbaya, anajua kukata majani ya Ng’ombe, kufagia zizi la ng’ombe anajua kulima, kufanya usafi, kupika na anakwenda sana kanisani.

Akasema kazi zote za nyumbani hufanya yeye, na watu wa hapa kijijini wanampenda sana. Akasema niachane na vibinti vya mjini kwani ni vivivu na havijui kufanya kazi na haviogopi mungu.

Kiukweli aliongea mengi lkn kubwa ni msisitizo kuwa nimuoee. Nilimjibu tutaongea na nitafikiria kwa kuzingatia kuwa, haitakuwa busara kumkatalia au kuanza kubishana nae.

Ilinibidi nianze kufuatilia nyendo za huyu dogo na nikagundua kuwa, hata yeye alikuwa tayari alikwishwa elezwa mpango huu.

Anyway, mkasa ndio huo, kuhusu kuoa au kutomuoa hilo sintalizungumza hapa ila habari kubwa niliyokutana nayo Kibosho ndio hii.

Tatizo La Nguvu za Kiume na Suluhisho.

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.

Katika kilele cha mwisho kabisa cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa.

Nguvu za kiume ni istilahi inayotumika mara nyingi kurejelea uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa kinyume chake, tunasema ni kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.

Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?

Kuishiwa nguvu za kiume ni tatizo la kawaida kwa wanaume. Ni hali ya kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.

Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).

Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.

Kwa wenye maradhi kama hayo ni bora kwanza kuwaona wataalamu wa tiba. Kwa ujumla, mtaalamu atafanya uchunguzi kimwili na maabara ya uchunguzi. Hii itaruhusu yeye kupata kushughulika vizuri juu ya tatizo, hali ambayo itamweka aendelee kutafiti chaguzi mbalimbali za tiba. Mhimu ni lazima kushauriana na daktari kwa ushauri juu ya matibabu ambayo ni bora.

Baadhi ya vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni pamoja na;
>Umri wa mgonjwa
>Jumla ya afya kwa sasa
>Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
>Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k

Ni nini malengo ya tiba ?
Kutafuta mtaalamu mzuri ni njia nzuri na ya kwanza katika kupata tiba sahihi. Ni mhimu kwanza wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako, kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya maradhi yanayokukabili.

Sababu zipi zinasababisha uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hujulikana kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii humwacha mwanamke akiwa hakuridhika. Mke wako hukutaka ukawie ikiwezekana ukawie zaidi. Kama mwanaume hataweza kukawia, basi anakuwa hampi raha mke wake.

Hata hivyo, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.

Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili na wakati huo huo zikiwa ni rahisi sana.

Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama vile;
>Wasiwasi
>Hofu
>Msongo/Stress
>Hasira
>Huzuni
>Ukosefu wa hamu katika mapenzi
Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea kama kipengele kimojawapo katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo. Pia sababu zingine za kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au kuwahi kufika kileleni ni pamoja na;
>Umri
>Maradhi ya kisukari
>Kujichua/Punyeto
>Uzinzi
>Ukosefu wa Elimu ya vyakula
>Kutokujishughulisha na mazoezi
>Shinikizo la juu la damu
>Maradhi ya moyo
>Uvutaji sigara/tumbaku
>Utumiaji uliozidi wa kafeina
>Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
>Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
>Kiwango kidogo cha testerone
>Kuumia kwa kinena (groin) au kuharibika

Athari kutoka kwa baadhi ya dawa ikiwa ni pamoja na madawa ya kwa ajili ya kutibu huzuni, maradhi ya moyo, shinikizo la damu na kifafa (epilepsy) na kadharika. Na madawa kama vile; Estrogen, Antiandrogens (flutamide), Lupron, Proscar, Diuretics, Methyldopa, Beta blockers, Calcium channel blockers, Tranquilizers (vitulizaji), Decongestants, Seizure medications, Madawa ya kupunguza kolesto, Cimetidine (dawa ya vidonda vya tumbo), Digoxin na kadharika.
Uhusiano wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Nini kinachofanya uume usimame?
Kwa haraka unaweza kujibu ni msisimko. Naam, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha msisimko huo. Bila hicho, msisimko hauwezi kutokea.

Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu sahihi la swali hili, ili atakapoona tatizo ajuwe pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama ilivyo dhana ya watu wengi.

Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.

Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ”Asilimia 94 ya damu ni maji”. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini na kama bado unasubiri kiu ndipo unywe maji na tena unakunywa maji ya baridi ya kwenye friji, POLE SANA

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika kusimama kwa uume wako.

Kwanini?

Mzunguko wa damu ulio katika afya njema husambaza damu ya kutosha katika viungo vyako vyote vya mwili wako ikiwa ni pamoja na kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kwamba hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako inavyostahili. Tazama mtu aliyekufa, damu haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano wa juu zaidi.

Ina maana kwamba, chochote ambacho huzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa yako ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume. Hii ni kwa sababu uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba sababu ya mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume walio na umri zaidi ya miaka 60, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye ateriosclorisis (hali ya ugonjwa inayosababishwa na kukauka kwa vijiateri vya ateri), na wenye maradhi ya moyo.

Kwa watu wengi, sababu ya kuishiwa nguvu za kiume ni mlo wa mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula vilivyosindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya ateri ina nafasi kubwa sana kutokana na kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni jambo la busara sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujenga utaratibu wa kuwa unajichunguza mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kutopendelea kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe taabani, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume:

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Vyakula vinavyotibu tatizo la nguvu za kiume ni pamoja na vifuatavyo;

Kitunguu swaumu
Chukuwa punje 10 mpaka 15 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.

Tikiti maji
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.

Ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote. Kama utahitaji unga huu wasiliana na mimi.

Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

Maji ya kunywa
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

Mbegu za maboga
Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako. Kama eneo ulipo hazipatikani waweza kuwasiliana na mimi.

Asali na Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja. Kama utahitaji asali wasiliana na mimi.

Unga unga wa udishe
Unga unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume.

Kuna matangazo mengi juu ya mitishamba inayoweza kutibu tatizo hili lakini naweza kukuhakikishia kuwa mti huu kweli unafanya kazi, utakupa nguvu sana hata kwa watu wenye umri mkubwa sana. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama. Chemsha maji nusu lita ongeza kijiko kidogo cha chai cha unga huu, unaweza kuongeza pia asali vijiko viwili na unywe kama chai kutwa mara mbili

Penzi La muuza Chips

Ni miaka miwili tu imepita baada ya kumaliza kidato cha nne, nilikuwa mwenye furaha kwa kuwa nilitamani kumaliza kidato cha nne nilikuwa nikiamini nitakuwa huru kwasababu wazazi wangu watanipa uhuru kwa kuwa nimeshakuwa mtu mzima sasa, lakini furaha yangu si kwa ajili hiyo tu bali nilijua baada ya kumaliza kidato cha nne nitafaulu na kuendelea na level nyingine (form v & vi) kitu ambacho nilitamani sana kwa sababu kwenye ukoo wetu wengi ni wasomi hivyo nilijitaidi nisiiangushe familia yangu kwa kuwa mtu wa kwanza kufeli kwenye fmilia yetu.

Kabla ya matokeo hayajatoka mama yangu mzazi aliamua anipeleke chuo nikasome kozi ya kingereza na kompyuta kwa muda ule ambao nasubiri matokeo. Kwa bahati mbaya nilipata kozi ya kingereza tu kutokana na upungufu wa fedha, nilijitaidi nijue kingereza kwa sababu niliamini nitakuwa na swagga na nitapendwa na wanawake wengi mtaani, maisha yaliendelea hivyo hivyo mpaka matokeo yakatoka lakini kwangu mimi hayakuwa mazuri sana nilipata division III ambapo post zilitoka serikalini ilichagua wale wa division I, II kuendelea na masomo ya juu. Nilisikitika sana na baada ya hapo niliwaomba wazazi wangu nikasome utangazaji sababu ndio kazi nilikuwa natamani kuja kuifanya lakini pia hilo lilishindikana kwa sababu familia yetu haikuwa na uwezo mkubwa hivyo kushidwa kunisomesha chuo kutokana na gharama kubwa zilizotakiwa.

Nilikaa nyumbani kwa mama kwa muda wa miezi sita bila kazi yoyote kweli maisha yalikuwa magumu ndipo kuna mjomba wangu alinisaidia kwa kunipa chumba ambacho alikuwa akiishi yeye na kisha akahamia kwenye nyumba yake mpya na kodi ilikuwa bado sana kuisha. Nilifurahi kukabidhiwa chumba kwa kuwa akili yangu iliwaza sana kula bata nikiwa huru, lakini upande mwingine maisha yatakuwa magumu zaidi ila nilijishauri tu liwalo na liwe mimi sijali. Mjomba alinipatia kiasi cha fedha ambacho ni mtaji wa biashara ambayo niliifikiria, kiukweli nilichukua muda mrefu sana kufikiria ni biashara gani nifanye ili maisha yaende sawa. Kusema ukweli niliwahi kuwaza hata ni wapi hapa nchini wanachukua watu kwa ajili ya kucheza video za X, nilihisi labda ningepata hela na burudani pia lakini mawazo yangu yaliishia kwenye biashara ya kuuza chipsi.

Niliona biashara hii ya chipsi itanifaa na nitafanikiwa, nilitafuta sehemu ambayo ningeweza kuanzisha biashara yangu nikapata maeneo ya sinza africasana. Bila kupoteza muda kesho yake niliingia sokoni kununua vitu vinavyohitajika pale kwenye biashara yangu. Karibu na nilipoanzisha biashara hii kuna shule inaitwa Kenton high school. Hivyo nilikuwa na uhakika wa kufanya biashara vizuri, kazi ilianza jumatatu ambapo nilitafuta msaidizi wangu ili tuweze kufanya kazi vizuri. Kusema ukweli kwa siku ile ya kwana nilipata wateja wengi sana na wengi wao walikuwa ni wanafunzi, walikuja wanafunzi wa aina mbalimbali muda ule wa saa nane nikawahudumia vizuri lakini baadae mida ya saa kumi kuna wanafunzi watatu wa kike walikuja pale kwenye biashara yangu, nilijisemea kimoyo moyo Kenton kuna watoto wazuri, niliwakaribisha wale wanafunzi kisha wakaagiza chipsi mayai nikawaandalia vizuri wakala. Nilishangaa sana walipomaliza kula wakaanza kunisifia chipsi zangu ni nzuri wakati ndio mara yangu ya kwanza kupika chipsi, lakini pia waliniahidi kuwa wateja wangu wa kudumu basi bila hiyana nikashukuru, nilijitambulisha naitwa Rommy na wao wakajitambulisha kusema ukweli nilitokea kumuelewa sana yule denti aliyejitambulisha kwa jina la Vicky…Alikuwa mzuri kuliko wote…ITAENDELEA