Tatizo La Nguvu za Kiume na Suluhisho.

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.

Katika kilele cha mwisho kabisa cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa.

Nguvu za kiume ni istilahi inayotumika mara nyingi kurejelea uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa kinyume chake, tunasema ni kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.

Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?

Kuishiwa nguvu za kiume ni tatizo la kawaida kwa wanaume. Ni hali ya kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.

Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).

Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.

Kwa wenye maradhi kama hayo ni bora kwanza kuwaona wataalamu wa tiba. Kwa ujumla, mtaalamu atafanya uchunguzi kimwili na maabara ya uchunguzi. Hii itaruhusu yeye kupata kushughulika vizuri juu ya tatizo, hali ambayo itamweka aendelee kutafiti chaguzi mbalimbali za tiba. Mhimu ni lazima kushauriana na daktari kwa ushauri juu ya matibabu ambayo ni bora.

Baadhi ya vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni pamoja na;
>Umri wa mgonjwa
>Jumla ya afya kwa sasa
>Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
>Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k

Ni nini malengo ya tiba ?
Kutafuta mtaalamu mzuri ni njia nzuri na ya kwanza katika kupata tiba sahihi. Ni mhimu kwanza wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako, kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya maradhi yanayokukabili.

Sababu zipi zinasababisha uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hujulikana kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii humwacha mwanamke akiwa hakuridhika. Mke wako hukutaka ukawie ikiwezekana ukawie zaidi. Kama mwanaume hataweza kukawia, basi anakuwa hampi raha mke wake.

Hata hivyo, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.

Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili na wakati huo huo zikiwa ni rahisi sana.

Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama vile;
>Wasiwasi
>Hofu
>Msongo/Stress
>Hasira
>Huzuni
>Ukosefu wa hamu katika mapenzi
Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea kama kipengele kimojawapo katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo. Pia sababu zingine za kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au kuwahi kufika kileleni ni pamoja na;
>Umri
>Maradhi ya kisukari
>Kujichua/Punyeto
>Uzinzi
>Ukosefu wa Elimu ya vyakula
>Kutokujishughulisha na mazoezi
>Shinikizo la juu la damu
>Maradhi ya moyo
>Uvutaji sigara/tumbaku
>Utumiaji uliozidi wa kafeina
>Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
>Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
>Kiwango kidogo cha testerone
>Kuumia kwa kinena (groin) au kuharibika

Athari kutoka kwa baadhi ya dawa ikiwa ni pamoja na madawa ya kwa ajili ya kutibu huzuni, maradhi ya moyo, shinikizo la damu na kifafa (epilepsy) na kadharika. Na madawa kama vile; Estrogen, Antiandrogens (flutamide), Lupron, Proscar, Diuretics, Methyldopa, Beta blockers, Calcium channel blockers, Tranquilizers (vitulizaji), Decongestants, Seizure medications, Madawa ya kupunguza kolesto, Cimetidine (dawa ya vidonda vya tumbo), Digoxin na kadharika.
Uhusiano wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Nini kinachofanya uume usimame?
Kwa haraka unaweza kujibu ni msisimko. Naam, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha msisimko huo. Bila hicho, msisimko hauwezi kutokea.

Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu sahihi la swali hili, ili atakapoona tatizo ajuwe pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama ilivyo dhana ya watu wengi.

Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.

Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ”Asilimia 94 ya damu ni maji”. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini na kama bado unasubiri kiu ndipo unywe maji na tena unakunywa maji ya baridi ya kwenye friji, POLE SANA

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika kusimama kwa uume wako.

Kwanini?

Mzunguko wa damu ulio katika afya njema husambaza damu ya kutosha katika viungo vyako vyote vya mwili wako ikiwa ni pamoja na kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kwamba hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako inavyostahili. Tazama mtu aliyekufa, damu haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano wa juu zaidi.

Ina maana kwamba, chochote ambacho huzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa yako ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume. Hii ni kwa sababu uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba sababu ya mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume walio na umri zaidi ya miaka 60, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye ateriosclorisis (hali ya ugonjwa inayosababishwa na kukauka kwa vijiateri vya ateri), na wenye maradhi ya moyo.

Kwa watu wengi, sababu ya kuishiwa nguvu za kiume ni mlo wa mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula vilivyosindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya ateri ina nafasi kubwa sana kutokana na kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni jambo la busara sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujenga utaratibu wa kuwa unajichunguza mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kutopendelea kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe taabani, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume:

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Vyakula vinavyotibu tatizo la nguvu za kiume ni pamoja na vifuatavyo;

Kitunguu swaumu
Chukuwa punje 10 mpaka 15 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.

Tikiti maji
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.

Ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote. Kama utahitaji unga huu wasiliana na mimi.

Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

Maji ya kunywa
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

Mbegu za maboga
Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako. Kama eneo ulipo hazipatikani waweza kuwasiliana na mimi.

Asali na Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja. Kama utahitaji asali wasiliana na mimi.

Unga unga wa udishe
Unga unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume.

Kuna matangazo mengi juu ya mitishamba inayoweza kutibu tatizo hili lakini naweza kukuhakikishia kuwa mti huu kweli unafanya kazi, utakupa nguvu sana hata kwa watu wenye umri mkubwa sana. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama. Chemsha maji nusu lita ongeza kijiko kidogo cha chai cha unga huu, unaweza kuongeza pia asali vijiko viwili na unywe kama chai kutwa mara mbili

One Reply to “Tatizo La Nguvu za Kiume na Suluhisho.”

  1. Hello. I have checked your nipenikupetz.com and i see you’ve got
    some duplicate content so probably it is the reason that you don’t rank hi
    in google. But you can fix this issue fast. There is a tool that generates content like human, just
    search in google: miftolo’s tools

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *